Thursday, August 2, 2012

Waasi wa M23 waelekea Goma

 

 


Wanajeshi wa serikali wakielekea mstari wa mbele kuulinda mji wa Goma.
Umoja wa Mataifa umefanya mkutano wa dharura hapo Jumanne (tarehe 31 Julai) juu ya kusonga mbele kwa waasi wa M23 kuelekea makao makuu ya mkoa huo, Goma. Baraza la Usalama pia linajadiliana kutoa taarifa ya kuwaonya waasi wanaosemekana kuungwa mkono na Rwanda.

Kwa mujibu wa wanadiplomasia katika Umoja wa Mataifa, Mjumbe Maalum wa Umoja huo kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Roger Meece, aliwapa wajumbe 15 wanachama wa Baraza la Usalama taarifa fupi inayoonya juu ya kitisho kipya kwa serikali ya nchi hiyo yenye utajiri wa rasilimali.

"Vikosi vya serikali vinaishiwa na silaha na wanaviacha vijiji mikononi mwa M23. Hii inazusha masuala kuhusu uwezo wa jeshi la serikali, kwani jeshi hilo limepata madhara makubwa sana." Alisema Meece kwa mujibu wa wanadiplomasia hao.

M23 waelekea Goma

No comments: