The Blue Point

Wednesday, April 22, 2015

Hong Kong na utata wa uchaguzi
Waandamanaji wanaotaka demokrasia mjini Hong Kong
Serikali ya Hong Kong imetangaza mapendekezo kukusu kuchaguliwa kwa kiongozi wa eneo hilo mwaka 2017.
Licha ya kushuhudiwa maandamano barabarani ya kuitisha demokrasia zaidi na mazungumzo ya muda mrefu mipango hiyo inasalia kuwa sawa na ile iliyotangazwa na China mwaka uliopita.
Wenyeji wa Hong Kong watawapigia kura wagombea lakini wagombea hao watahitajika kuidhinishwa na kamati kutoka China.
Wagombea wa nafasi hiyo ni lazima wapate uungwaji mkono wa asilimia kubwa ya kamati ya uteuzi ambayo itawajumuisha wanachama wa chama cha kikomisti.
Hata hivyo mpango huo haukubaliki na baadhi ya wapiga kura nchini Hong Kong ambao wanataka uchaguzi wa wagombea ulio huru.CHANZO:BBC (Muro)

Monday, April 20, 2015

Chama Kikuu cha Upinzani Chashinda Finland


Rais mteule wa Finland Juha Sipila
Rais mteule wa Finland Juha Sipila
Baada siku kadhaa kupita kwa chama kikuu cha upinzani cha  Nigeria APC kuchukua madaraka mabadiliko hayo yameonekana kuendelea kushuhudiwa katika nchi nyingine katika nchi ya Finland Chama kikuu cha upinzani cha CP kimeshinda uchaguzi kwa kunyakuwa asilimia 21.1 ya kura zote zilizopigwa huku chama tawala kikipata asilimia 16.5.
Kwa mujibu wa matokeo yasiyokuwa rasmi, chama cha CP kimeshinda viti 49, SF viti 37, SD viti 34, DG viti 15, SP viti 38, Left Party viti 12, SFP viti 9, KD viti 5 na chama cha kujitegema kiti 1 kati ya viti 200 vya bungeni.
Mwenyekiti wa chama cha CP Juha Sipila, alitangaza ushindi wake baada ya asilimia 98.3 ya kura kuhesabiwa.
Sipila alitoa shukrani zake kwa wananchi wa Finland.
Matokeo ya chama tawala yaliwashangaza watu wengi lakini imearifiwa kuwa Matokeo mabaya ya chama hicho yalichangiwa na kuzorota kwa uchumi na ongezeko kubwa la ukosefu wa kazi nchini humo.Na mitandao ya habari.

Zanaki yazidi ‘kutesa’


Zanaki imeshika nafasi ya pili kwa darasa la saba kati ya shule 167 za msingi za serikali.
Zanaki imeshika nafasi ya pili kwa darasa la saba kati ya shule 167 za msingi za serikali.
Shule ya Msingi Zanaki, iliyopo Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam imeendelea kuongoza kwa ubora kitaaluma kwa mwaka wa pili mfululizo baada kushika nafasi ya pili kwa darasa la saba kati ya shule 167 za msingi za serikali.
Pia Zanaki imeshika nafasi ya kwanza kwa ubora katika mitihani ya darasa la pili ikiongozwa na Msimbazi Mchanganyiko kwa shule zote za msingi katika manispaa hiyo.
Akitanganza ushindi wa Zanaki, Afisa Elimu Msingi wa Manispaa hiyo, Elizabeth Thowa, alisema shule hiyo imeendelea kuwa kinara kitaaluma baada ya wanafunzi wake kupata alama nyingi za A na B kwa masomo yote.
Zanaki imeshika nafasi ya kwanza kwa ubora katika mitihani ya darasa la pili ikiongozwa na Msimbazi Mchanganyiko
Zanaki imeshika nafasi ya kwanza kwa ubora katika mitihani ya darasa la pili ikiongozwa na Msimbazi Mchanganyiko
Alisema Zanaki imefanikiwa kushika nafasi ya 10 kwa ubora kitaaluma kwa kushirikisha shule zote za serikali na binafsi kwa darasa la saba, huku ikishika nafasi ya nne kwa ubora wa mitihani ya darasa la nne kwa shule zote.
Thowa alikuwa akizungumza wakati wa kilele cha wiki ya Elimu na Mazingira ya manispaa hiyo, iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambako shule za msingi na sekondari za serikali na binafsi zilishiriki na kutunukiwa zawadi ya vyeti, vikombe na vifaa vya usafi.
Mapema akizungumza katika hafla hiyo iliyotanguliwa na maandamano yaliyopokelewa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, Afisa Elimu (Sekondari), Violet Mlowosa, alisema maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kujengea hamasa wanafunzi na walimu kufanya bidii kitaaluma na kutunza mazingira.
Moja ya mazingira ya shule ya msingi Zanaki
Moja ya mazingira ya shule ya msingi Zanaki
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Zanaki, Salim Mgamba, alisema shule yake itaendelea ‘kutesa’ kitaaluma kwa sababu wazazi na walezi wanasaidia kila kinachohitajika, hivyo kuwarahisishia walimu na viongozi wa elimu manispaa hiyo kutimiza majukumu yake.
Chanzo: NIPASHE

Sunday, April 19, 2015

Ray C AFUNGUKA kuhusu wimbo mpya wa Lord Eyez ambao kashirikishwa

 


ray c 3
Wiki mmoja baada ya taarifa za wimbo mpya wa rapa wa Weusi Lord Eyez ambao kashirikishwa Ray C kuripotiwa kutoka hivi karibuni, Ray C ametumia instagram yake kutufahamisha kuwa huu ni wimbo wa zamani waliorekodi nchini Kenya.

Machafuko Afrika KusiniGhasia za kuwashambulia wageni zilizoanza Durban wiki mbili zilizopita zimesababisha vifo vya Watanzania wawili
Ghasia za kuwashambulia wageni zilizoanza Durban wiki mbili zilizopita zimesababisha vifo vya Watanzania wawili
Watanzania wawili wanaoishi Afrika Kusini wameuawa kwa kile kinachohusisha muendelezo wa hofu na chuki dhidi ya wageni ambao umetikisa hivi karibuni.
Taarifa ya vifo imekuja baada ya Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernard Membe, kutangaza kutoka Oman kwamba Tanzania imeanza kuondoa raia wake kutoka Yemen ambapo kumekumbwa na vita ya umwagaji damu baina ya majeshi ya serikali na waasi.
Wageni wakiwa na silaha za jadi tayari kupamba na wenyeji waliokuwa wakivamia maduka yao mjini Durban
Wageni wakiwa na silaha za jadi tayari kupamba na wenyeji waliokuwa wakivamia maduka yao mjini Durban
Nchini Afrika Kusini, mwakilishi wa Watanzani waishio nchini humo aliiambia The Citizen jana, kwamba watu wawili wameuawa katika ghasia za kushambulia wageni ambazo zimesababisha vifo vya watu watano kutoka mataifa mengine na kuwakoseasha makazi maelfu katika mji wa Durban.
Bw Bonka Kusekela, mwakilishi wa Watanzania, alitaja majina ya marehemu kama Rashid Jumanne, muuza sigara ambaye aliuawa Jumanne huko Stenga, mtaa uliopo Durban na mwingine ni Athumani maarufu kama China Mapepe, ambaye aliuawa Jumanne katika jiji kubwa la jimbo la KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.
Jamaa akiwa na panga huku akishangiliwa na wenzake mjini Johannesburg
Jamaa akiwa na panga huku akishangiliwa na wenzake mjini Johannesburg
Kwa mujibu wa Kusekela, Rashid alipigwa risasi na mtu asiyejulikana wakati akifanya biashara yake wakati Athumani, mfungwa katika gereza kurekebisha makosa la Westville alichoma kisu hadi kufa na wafungwa wenzake.
“Ninavyozungumza nanyi sasa tuko katika maandamano ya amani na baadhi ya wenyeji mjini Durban kulaani mauaji haya ya kikatili lakini tumeshapoteza Watanzania wawili mpaka sasa,” aliiambia The Citizen kwa simu kutokea Durban.
Mtuu mmoja akiwa ameshika jiwe kufuatia ghasia hizo ambazo zimesababisha vifo vya watu watano
Mtuu mmoja akiwa ameshika jiwe kufuatia ghasia hizo ambazo zimesababisha vifo vya watu watano
Lakini kwa majibu ya haraka, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Elibariki Ngoyai Lowassa alisema hakuna taarifa rasmi kwamba watu wawili wamefariki kutokana muendelezo wa ghasia dhidi ya wageni.
Akizungumza na The Citizen kutoka Afrika Kusini, hatahivyo, Bw Lowassa, alithibitisha vifo vya Watanzania wawili.
Polisi wa Afrika Kusini wakitumia risasi za plastiki kutawanya magenge ya wahamiaji waliokuwa wakipambana nao
Polisi wa Afrika Kusini wakitumia risasi za plastiki kutawanya magenge ya wahamiaji waliokuwa wakipambana nao
Chanzo: The Citizen

Dk. Mengi ahofia maisha yake


Mwenyekiti mtendaji wa IPP Dr. Reginald Mengi ameeleza kushtushwa na taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la taifa imara zikimtuhumu kuwa ana nia ya kutaka kuiangusha serikali ya Rais Kikwete na kumshughulikia baada ya kumaliza muda wake wa uongozi kunyamaziwa na ikulu na idara ya habari maelezo kwa wiki tatu bila kutoa ufafanuzi wowote
Mwenyekiti mtendaji wa IPP Dr. Reginald Mengi ameeleza kushtushwa na taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la taifa imara zikimtuhumu kuwa ana nia ya kutaka kuiangusha serikali ya Rais Kikwete na kumshughulikia baada ya kumaliza muda wake wa uongozi kunyamaziwa na ikulu na idara ya habari maelezo kwa wiki tatu bila kutoa ufafanuzi wowote
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi amesema anahofia usalama  wa maisha yake, kufuatia habari iliyoandikwa katika gazeti moja la kila wiki  kwamba,  Rais Jakaya Kikwete aliapa kupambana naye jambo ambalo limempa hofu kubwa.
Kadhalika, amelalamikia  Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu na Idara ya Habari Maelezo kwa kukaa kimya na kuacha kutoa ufafanuzi dhidi ya tuhuma hizo, huku taarifa hizo zikiendelea kusambazwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mengi alisema kuwa tuhuma zilizotolewa dhidi yake kuwa yeye ni kinara wa kuhujumu serikali ya Rais Kikwete siyo za kweli.
Dk. Mengi alisema amesoma kwa masikitiko makubwa habari iliyochapishwa Machi 23, mwaka huu na gazeti la Taifa Imara, yenye kichwa cha habari ‘Zitto amchongea Mengi kwa JK’ ambapo pamoja na mambo mengine inasema kuwa Zitto Kabwe amemchongea Dk. Mengi kwa Rais Kikwete kwamba ndiye kinara wa kuhujumu serikali yake.
Alisema habari hiyo ambayo chanzo chake kimeelezwa kwamba ni Ikulu, iliendelea kueleza kuwa Zitto alikutana na Rais Kikwete muda mfupi baada ya kuwasilisha bungeni ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusiana na kashfa ya Escrow ambayo Zitto alikuwa ni mwenyekiti wake.
“Habari hiyo inasema kwamba katika mazungumzo yake na Rais Kikwete Zitto amenukuliwa akimueleza mkuu huyo wa nchi kuwa anayesababisha serikali yake iyumbe kila mara ni Mengi,” alisema Dk. Mengi.
Dk. Mengi alisema habari hiyo ambayo nakala yake ameiambatanisha kwenye taarifa yake, inasema yeye Zitto , binafsi amekuwa akishawishiwa na Dk. Mengi kuiangusha serikali ya Rais Kikwete.
Hata hivyo, Dk. Mengi alisema katika habari hiyo Zitto alikwenda mbali zaidi kumueleza Rais Kikwete kuwa Dk. Mengi ameapa kuwa Rais Kikwete akimaliza muda wake wa Urais atamshughulikia kwa nguvu zake zote.
Alisema habari hiyo imeeleza kwamba baada ya maelezo hayo, Rais Kikwete aliapa kupambana na Dk. Mengi na akamshukuru Zitto kwa kumpa taarifa hizo.
Mengi alisema tuhuma zilizotolewa kuhusu nia yake ya kutaka kuiangusha serikali ya Rais Kikwete na kumshughulikia baada ya kumaliza muda wake wa uongozi, zimemshtua sana na tamko la kwamba Rais Kikwete aliapa kuwa atapambana na yeye zimempa hofu kuhusu mustakabali wa maisha yake.
Alisema kuwa hofu yake kubwa inasababishwa na Ikulu na Idara ya habari Maelezo kukaa kimya kwa zaidi ya wiki tatu bila kutoa ufafanuzi wowote.
“Najua umakini wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu na Idara ya habari Maelezo katika kutoa ufafanuzi wa haraka wa jambo lolote linalomhusu Rais, lakini katika hili nashangaa kuona taasisi hizo zimeamua kukaa kimya na kuacha tuhuma hizo kusambaa,”alisema Dk. Mengi.
Aliongezea kusema kuwa,” hofu yangu inazidi kuwa kubwa kwa sababu Rais ni Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama. Kauli yake kama ilivyonukuliwa na gazeti hili kwamba atapambana na mimi inawezekana kuchukuliwa kama agizo kwa vyombo vya dola kuniangamiza,” alisema.
Alitolea mfano mwaka 1170, Askofu Mkuu wa Canterbury nchini Uingereza aliuawa baada ya walinzi wa mfalme kusikia mfalme akisema “hakuna anayeweza kuniondolea huyo mkorofi?”. Walinzi wake wakadhani mfalme ameagiza wamuue Askofu huyo na wakamuua, alisema.
Chanzo: NIPASHE

APNewsBreak: Video released of 'Suge' Knight running over 2


April 18, 2015 2:49amThursday, April 16, 2015

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF limeitakia kheri timu ya Young AfricansRais wa TFF, Jamal Malinzi
Rais wa TFF, Jamal Malinzi
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi ameitakia kila la kheri timu ya Young Africans katika mchezo wake wa jumamosi wa Kombe la Shirikisho barani Afrika (CC) dhidi ya timu ya Etoile du Sahel kutoka Tunisia, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar  es Salaam.
Katika salamu zake kwa klabu ya Young Africans, Rais Malinzi amewaambia wanapaswa kupambana na kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo wa jumamosi, ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele katika mchezo wa marudiano kwani ndio pekee kwa sasa wanaoipeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya kimataifa.
Young Africans imeingia katika hatua ya 16 bora Kombe l Shirikisho barani Afrika,baada ya kuzitoa BDF XI ya Botswana katika hatua ya awali kwa jumla ya mabao (3-2), kisha kuwaondoa FC Platinum ya Zimbabwe katika hatua ya kwanza kwa jumla ya mabao (5-2).
Endapo timu ya Young Africans itafanikiwa kuwaondoa Etoile du Sahel itasuburia kucheza  mechi ya mtoano (Play-off) dhidi ya timu mojawapo zitakaotolewa katika 16 bora ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CL).
Wakati huo huo wapinzani wa Young Africans timu ya Etoile du Sahel wanatarajiwa kuwasili  saa 9 usiku kuamkia ijumaa kwa usafiri wa Ndege ya kukodi ya kampuni ya Nouvelair   bj 4870 wakiwa na msafara wa watu 56.
Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Yanga
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tunisia  (FTF), Bw. Krifa Jalel ndiye mkuu wa msafara huo akiwa na Rais wa klabu ya Etoile du Sahel (ESS) Bw.Charefeddine Ridha, wachezaji 19, benchi la ufundi lenye watu 13, waandishi wa habari 12 na wanachama 10
Timu ya Etoile du Sahel itafikia katika hoteli ya Ledger Plaza zamani Bahari Beach eneo la Kunduchi, na kesho jioni ijumaa wanatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Waamuzi wa mchezo huo ni Samwel Chirindiza, Arsenio Marenguka, Celio de Jesus Musabe, Jose Maria Bachide wote kutoka nchini Msumbuji na wanatarajiwa kuwasili leo mchana, huku kamisaa wa mchezo huo Salah Ahmed Mohamed kutokea nchini Sudan akitarajiwa kuwasili leo jioni na wote watafikia katika hoteli ya Protea iliyopo Oysterbay.

TAARIFA KUTOKA TUMA YA TAIFA YA UCHAGUZI Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini Tanzania itaanza kusambaza mashine za BVR 248 katika mikoa saba nchni Tanzania Kuanzia katikati mwa wiki ijayo.
Mikoa iliyopangwa kuanza kupokea mashine hizi ni mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa, Wakati zozi likianza mikoa hiyo nyingine zitakuwa zinapelekwa katika mikoa ya Katavi, Mbeya na Dodoma. Mikoa mimgine ni Singida Tabora Geita na Kigoma.
Mkuu wa kitengo cha Ufundi wa idara ya Daftrari/ICT wa NEC Dr Sisit Cariah, Akizungumza na mwandishi wetu amesema kwamba mpaka sasa wanachi wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvumna na Iringa wakae tayari kwani muda wowote watatangaziwa vituo vya kujiandikisha.
 Pamoja na mshine hizo 248 Tume ya taifa ya uchaguzi imewaandaa wataalamu 248 ambao watakuwa na jukumu la kutoa elimu kwa wataalamu wengine 50 kwa kila mmoja nchi nzima kwa ajili ya kuharakisha uandikishaji kwa mfumo wa BVR.
Dr Sisit Ameeleza kwamba wamefanikiwa kufanya maboresho makubwa katika mashine hizi ikiwa ni pamoja na kubadilisha upangaji wa vifaa (settings), mfumo endeshi (Software) na upande wa Vichapishio (printer) ambazo sasa zimetengenezewa Nchini Ufaransa umeboreshwa na nirahisi kusafishwa.

Mafunzo yaliyoendeshwa hapa Jijini Dar es Salaam yamechukua siku moja na yamezingatia sana upande wa Vichapishio (printer), Visoma alama za vidole (Finger Print Scaner) na Kamera kutambua macho mekundu. Ameongoza kwamba printer za sasa ni rahisi kusafishwa na hata kuweka kifaa kipya baada ya cha zamamni kuharibika vimerahisishwa.
Kuhusu uchukuaji wa alama za vidole, amesema kwamba kwa sasa tatitzo la mashine ya kuchukua alama za vidole wamelifanikisha kwa asilimia mia. Kwani kwa wale ambao hawana alama za vidole mashine zimewekewa mfumo wa alogarithim mpya ambao uatatambua kila aina ya kidole.
Hata hivyo Kamera zimewekewa mfumo mpya wa kutambua macho mekundu na kurekebisha rangi ya macho mekundu (Red eyes) Bila kukwamisha zoezi la uandikishaji.
Mtarajio ni kwamba zoezi lauandikishaji liwe limekamilika ndani ya kila siku 28 tokea kila mkoa unapopokea mashine hizi. Vilevile Dr Sisit ameishukuru serekali kwa kufanikisha upatikanaji wa Vifaa “serekali imejitahidi kuandaa upatikanaji wa mashine hizo, na usafirishaji kwa njia ya ndege kwenda nchi nzima. Kila halmashauri na mkoa utachukua angalau siku 28 kukamilisha mkoa utakapo pokea Vifaa” Dr Sisit amesema.
Mwisho amesema kwamba mashine nyingine 1,600 zitawasili wakati wowote na kwamba serikali imetoa Dola za Marekani milioni 72 (Sh. bilioni 133).
Kuwasili kwa mashine hizo, kunaifanya Nec kupokea mashine 2,098, huku ikisubiri mashine 5,902, ili kukamilisha 8,000 zinazotakiwa. Alisema vifaa hivyo vinanunuliwa na serikali kupitia kampuni ya Lithotech Export ya Afrika Kusini, ambayo imeingia mkataba na Nec na inaviagiza China.Sourcehttp://www.hakingowi.com

Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini-Chadema Philemoni Ndesamburo Atangaza Rasmi Kutogombea Tena Jimbo la Moshi Mjini Amnadi Mrithi Wake
 Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akiwasili katika viwanja eneo la soko la Manyema akiwa ameongozana na Diwani wa kata ya Mji Mpya ,Abuu Shayo na Stephen Ngasa wa kata ya Kiusa.
 Ndesamburo akizungumza na wananchi wa Moshi mara baada ya kumtangaza mrithi wake katika jimbo la Moshi mjini.
 Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akimtambulisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Jafary kuwa mrithi wake wa kiti cha ubunge katika jimbo hili wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba.
 Mstahiki Meya a manispaa ya Moshi,Jafary Michael akihutubia mamia ya wananchi waliofika katika mkutano huo uliofanyika katika viwanja vilivyoko jirani na soko la Manyema .
 Mmoja wa wafuasi wa Chadema akiwa amekaa chini akifuatilia mkutano huo.
 Mamia ya wananchi katika mji wa Moshi wakishangilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Msathiki Meya wa manispaa ya Moshi,Jafary Michael.

 Mamia ya wananchi wakimsikiliza Ndesamburo.
 Baadhi ya wakazi wa mji wa Moshi wakifuatili mkutano wa hadhara wa Chadema uliofanyika katika eneo la soko la Manyema.
 Katibu mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Moshi na Diwani wa Kata ya Kiusa ,Stephen Ngasa akizungumza katika mkutano huo wa hadhara.
 Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini ,Philemoni Ndesamburo akiteta jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Clement Kwayu wakati wa mkutano wa hadhara.
Mstahiki Meya ,Michael akiwa amekaa kando ya Mbunge ,Philemoni Ndesamburo .
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.